Matokeo kamili kama yalivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), yanaonesha licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia, mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad alipata kura 6,076 kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili.
Hamad Rashid Mohamed wa chama cha ADC ndiye wa pili akiwa na kura 9,734.
Baadhi ya waliowania urais wamefika ukumbini na kuketi. Mmoja wao ni mgombea wa ADC Hamad Rashid.
Wanahabari, waangalizi na maafisa wengine wa uchaguzi wakiwa ukumbini wakisubiri kuanza kutangazwa kwa matokeo.
No comments:
Post a Comment