ZIJUE FAIDA ZA KULA MATANGO (CUCUMBERS)
Tango ni tunda moja wapo yenye maji mengi kama vile tikiti maji ,linabeba virutubisho vingi vitamin K,B,C,potasium,manganese .
Tango lina polyphenols ambayo inasaidia kukuepusha kupata maradhi
sugu. Ni vizuri mkatumia matanga mara kwa mara kwa kutengeneza
juice,kuchanganya kwenye kachumbali (salad)bila kumenya maganda yake
yanabeba virutubisho vizuri,au unaweza weka kwenye mkate na kuchanganya
na maji ya kunywa kuyapa ladha na vitamins.

Umuhimu wa kula tango kwa afya yako
1.Kuupa ubongo kinga
Tango lina anti-inflammatory flavonol inayopelekea kuupa ubongo kinga
na kukufanya kuwa na kumbukumbu nzuri (improve your memory).
2.Kupunguza hatari ya kupata cancer.
Tango linakupunguzia hatari ya kuapata cancer ya maziwa na shemu za uzazi (uterine,mayai ya uzazi (ovari).
3.Kutoa harufu mbaya mdomoni.
Kata kipande cha tango weka mdomoni kwa dakika 5 fanya mara 3 kwa siku inataidia kutoa bakteria wafanya kunuka mdomo .
4.Kupunguza stress
Tango linavitamins B,vitaminB1 vitaminB5 na vitamini B7 ambazo zinakupunguza stress.
5.Kusaidia mmeng’enyo wa chakula.
Tango lina maji maji na fiber inayosaidia mmeng’enyo wa chakula
tumboni,kwa wale wenye tatizo la kupata haja kubwa(constipation) kula
tango bila kumenya ganda lake, linabeba fiber itakayo kusaidia kuapa
choo kwa urahisi.
6.Wenye matatizo ya moyo
Tatizo la pressure linaweza kupunguzwa kwa kula matango mara kwa
mara sababu tango lina potasium inayofanya kushuka pressure kwa urahisi
na salama.
7.Kupunguza hatari ya kupata kisukari,kupunguza cholesterol
8.Kutibu maumivu ya viungo
9.Kufanya kuwa na ngozi laini na kukuza nywele kwa haraka.
10.Kupunguza uzito
11.Kutumika kutoa alama nyeusi chini ya macho
Kata tango umbo la duara weka kipande kimoja kwa kila jicho, fanga
macho ndio uweke kwa juu . Kwa matumizi ya uso(facial ) pia unasaga iwe
laini (puree) na paka usoni acha kwa dakika 20 ,kish nawa kwa maji safi
itakufanya kuwa soft na fresh.
12.Kutoa sumu mwilini
tengeneza juice ya tango,unaweza changanya na apple,spinachi na
limao saga pamoja ni njia nzuri ya kutoa sumu mwilini kwa wale
wanaotumia madawa kali n.k
No comments:
Post a Comment