Friday, April 8, 2016

BAJETI 2016/17 ISISAHAU WALEMAVU


 Wito huo umetolewa leo na Josephine Bakhita, Ofisa Ustawi wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Erick inayojihusisha na watu wenye ulemavu wa akili (EMFRED) wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Bakhita ambaye pia alikuwa na mtoto mwenye ulemavu huo Erick Bakhita na kufariki dunia, ameeleza kuguswa na kuamua kufungua kituo hicho ili kusaidia jamii ya walemavu hao.
Bakhita amesema kuwa, jamii hiyo imekuwa haifikiwi kwa haraka na kwamba, hata watunga sera bado hawajaanza kuangalia mbinu za kuwaibua na kuweka utetezi juu yao ili waweze kupata haki zao za msingi kama wanadamu wengine wanavyopata.

Amesema kuwa, tangu taasisi hiyo ianzisha Mei 2011 hadi Desemba 2015 tayari imeweza kusajili familia 637 zenye jamii ya walemavu katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Gairo na Mvomero.
“Kilio changu kikubwa ni kwa walemavu hasa wa akili, ni kundi kubwa linalotengwa na kuminywa kwenye jamii kutokana na wazazi husika kutokuwa na elimu na serikali kutolivalia njuga suala hilo,” Amesema.

Esther Andrew (40), Mkazi wa Malolo, Kilosa ambaye ni mama wa mtoto Grace Emmanuel (15) mwenye ulemavu wa akili kituoni hapo ameiomba serikali kusaidia kituo hicho.

No comments:

Post a Comment