Tuesday, March 22, 2016

MLIPUKO WAUA 26 KATIKA UWANJA WA NDEGE BRUSSELS-UBELGIJI

Moshi ukifuka katika uwanja wa ndege wa Zaventem jijini Brussels, Ubelgiji muda mchache baada ya kutoka milipuko
Watu 26 wamefariki baada ya mashambulio kutekelezwa katika uwanja wa ndege wa Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek mjini Brussels.
Waziri wa afya wa Ubelgiji amesema watu 11 walifariki na wengine 81 kujeruhiwa baada ya milipuko miwili kutokea uwanja wa ndege wa Zaventem, nje kidogo ya mji wa Brussels.
Kampuni inayosimamia uchukuzi wa treni Brussels imesema kwamba watu 15 walifariki Maelbeek na wengine 55 kujeruhiwa, 10 kati yao wakijeruhiwa vibaya.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Francois Hollande amelaani mashambulio hayo mjini Brussels na kusema ni kama mashambulio yaliyolenga bara lote la Ulaya.
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema hatua zaidi zimechukuliwa kuimarisha usalama mpakani

No comments:

Post a Comment