Friday, March 25, 2016

RAIS DR. SHEIN AAHIDI KUSIMAMIA MISINGI YA HAKI NA UADILIFU KATIKA SERIKALI YAKE



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Ali Mohamed Sein ameahidi Serikali yake mpya atakayoiunda itafuata Misingi ya Haki na Uadilifu na hakuna mtu atakayebaguliwa .
Dkt.Shein pia ame ahidi kuwa Seriklai yake itashirkiana na vyama vya siasa vya upinzani katika kujenga serikali mpya .
 
Hiyo itahusu zaidi utekelezaji wa Ilani ya chama chake cha Mapinduzi yenye vipenge vinne  vya ajira,mapambano dhidi ya umaskini,rushwa na kulinda umoja wa kitaifa.
 
Ameyasema hayo baada ya kuapishwa kuwa  kiongozi wa Zanzibar kwa awamu ya saba kipindi cha pili.
 
Wakati wa kuapishwa dua zilizosomwa na viongozi wa dini wa madhehebu mbali kabla ya kupanda kwenye jukwa kupokea salamu za rais na kupandishwa kwa bendera ya rais.
 
Baadaye alikagua Gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na majeshi ya ulinzi na usalama kabla ya kutoa hotuba yake kuhusu awamu ya pili ya uongozi wake.
 
Miongoni mwa waliohudhuria sherehe ya kuapishwa kwake kwenye Uwanja wa Aman Zanzibar ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu,Kassim  Majaliwa na viongozi mbalimbali  wastaafu.

No comments:

Post a Comment