Friday, March 25, 2016

Jeshi la Polisi DSM limesema limejipanga vema kuhakikisha ulinzi unaimarika Sikukuu ya Pasaka.




Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imesema imejipanga vema kuhakikisha usalama unakuwepo wakati wa sikukuu ya pasaka na kuonya wale wenye nia mbaya yakufanya vitendo vya uharifu katika kipindi hicho na kuhatarisha amani.

Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salam CP.Simon Sirro amezungumza hayo wakati wa mahojiano maalum na ITV kuhusu hali ya usalama wakati wa Sikukuu ya Pasaka na kusema kila mmoja atii sheria bila shuruti ili asije akanaswa na vyombo vya Dola kwa kuvunja sheria na taratibu mbalimbali za nchi.

No comments:

Post a Comment