Serikali wilayani Bariadi Mkoani Simiyu imewasimamisha kazi
Watumishi watatu wa Halmashauri ya Bariadi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo
ya walimu kuuziwa vitambulisho vya kazi,fomu ya (OPRAS) na walimu 22
waliosimamishwa na kurudishwa kazini na kushindwa kulipwa madai yao ya
miaka mitatu kiasi cha milioni 150 baada ya kuagizwa na Tume ya walimu
TSD na kukaidi kufanya hivyo.
Uamuzi wa kuwasimamisha kazi Watumishi hao umekuja muda mfupi baada
ya kumalizika kwa kikao cha pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya hiyo Ponsiano
Nyami na waalimu zaidi ya elfu moja wa Wilaya ya Bariadi
kilichofanyika katika Ukumbi wa Bariadi Motel ambapo walipomueleza mkuu
huyo namna wanavyonyanyasika na watumishi hao kiasi cha kukata tamaa,ya
kufundisha kutokana na madai yao yakiwemo malimbikizo ya mishahara.
Mara baada ya kikao hicho Mkuu wa Wilaya akaitisha kikao cha
dharura cha Kamati ya Ulinzi na Usalama,ambapo akatoa kauli ya
Serikali ya kuwasiamamisha Watumishi hao mbele ya waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment