Friday, March 25, 2016

WANASAYANSI WATHIBITISHA NAMNA POVU LA CHURA LINAVYOWEZA KUTIBU VIDONDA




Chura

Povu linalotengenezwa na vyura wadogo kwa ajili ya kulinda mayai yao linaweza kuponya majeraha ya wagonjwa walioungua, wanasema wanasayansi.
Povu gumu linaweza kukusanywa na kutumiwa katika mchakato wa matibabu kama kizuizi baina ya bandeji na ngozi iliyoungua.

Watafiti katika Chuo kikuu cha Strathclyde wameanza majaribio ya sehemu ya povu hilo.
Wanafanya majaribio hao kwa kutumia povu kutoka kwa vyura hao wadogo kutoka kisiwa cha Tungara huko Trinidad.
Vyura hao kutoa povu la urefu wa sentimeta 5 kulinda mayai yao dhidi ya magonjwa na hali ya hewa kwa wastani wa siku tano.
Povu hilo imetengenezwa kwa aina tano za Protini.
Doctor Paul Hoskissonna wenzake wanasema wameweza kuzichunguza aina nne za protini hizi na wameanza kuzichanganya na dawa zao.
Watafiti hao watawasilisha kazi yao katika katika mkutano wa mwaka wa kituo cha uratibu wa shughuli za utafiti wa viumbe hai -Microbiology Society utakaofanyika Liverpool.

No comments:

Post a Comment