Friday, March 25, 2016

WASHUKIWA SITA WA SHAMBULIO LA BRUSSELS-UBELGIJI WAKAMATWA



Polisi nchini Ubelgiji wamewakamata washukiwa sita mjini Brussels huku uchunguzi ukiendelea kuhusu mashambulio ya Jumanne yaliyosababisha vifo vya watu 31.
Watu hao walikamatwa katika mtaa wa Schaerbeek.
Polisi bado hawajatoa majina yao na pia hawajasema iwapo walihusika katika mashambulio hayo.
Kwingineko Ufaransa, mshukiwa ambaye inasadikika alikuwa akipanga shambulio amekamatwa karibu na mji wa Paris, maafisa wamesema.
Mashambulio hayo ya Brussels yamehusishwa na mashambulio ya Paris ya Novemba mwaka jana.
Kundi linalojiita Islamic State (IS) limekiri kutekeleza mashambulio yote mawili

No comments:

Post a Comment